Jumanne 18 Novemba 2025 - 17:29
Ushindi wa Iran katika vita vya siku 12 umetokana na uwezo wa ndani na uongozi wenye hekima

Hawza/ Imamu wa Ijumaa wa Michigan ameeleza kuwa ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vita vya siku kumi na mbili ni ishara ya kutegemea uwezo wa ndani pamoja na uongozi wenye hekima wa Ayatullah Khamenei. Pia alionya kwamba leo tishio kuu kwa Iran linatokana ndani ya nchi.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Basim al-Shar‘, Imamu wa Ijumaa wa Michigan nchini Marekani, katika khutba za Ijumaa zilizopita alisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika vita vya siku kumi na mbili ambavyo utawala wa Kizayuni ulivilazimisha dhidi yake, “ilivuna ushindi wenye kung’aa” na iliweza kutetea maslahi yake ya kitaifa bila kutegemea nguvu za mataifa ya kigeni.

Al-Shar‘, akirejea miaka zaidi ya minne ya mashinikizo na vikwazo dhidi ya Iran, alisema: “Iran, licha ya miaka arobaini ya kuzingirwa na bila ya msaada wa China, Urusi au nchi nyingine yoyote, kwa kutegemea uzalishaji wa ndani, maamuzi ya busara na uimara wa wananchi wake, iliweza kuondoa tishio la nje kwa ujasiri na umakini.”

Imamu wa Ijumaa wa Michigan aliendelea kueleza kuwa; vituo vya utafiti na uchambuzi duniani vinachunguza namna ushindi huu ulivyopatikana, na kwamba nafasi ya uongozi katika mafanikio haya imepewa umuhimu maalumu.

Akaongeza kuwa: “Kiongozi wa Mapinduzi, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni shakhsia ya kimataifa ambayo vituo vya kimataifa huitilia maanani kauli na misimamo yake. Hekima, wepesi wa kufanya maamuzi na uwezo wa kusimamia mitikisiko ya kisiasa ni miongoni mwa sifa zilizomfanya kiongozi huyu mkubwa awe bado akiheshimiwa duniani akiwa na umri wa miaka tisini.”

Al-Shar‘, akionesha masikitiko yake kuhusu kuzuka kwa ukosoaji fulani ndani ya Iran baada ya kumalizika kwa vita, alitaja tabia hiyo kuwa “chanzo cha changamoto na yenye kudhuru”, na kusema: “Cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya viongozi wa zamani wa serikali kuu ya Iran, ambao kwa miaka mingi walikuwa katika nafasi za madaraka, baada ya kumaliza kipindi chao wameanza kuleta dhana potofu na kutoa vijembe dhidi ya uongozi; jambo hili linaathiri afya ya mazingira ya ndani ya Iran.”

Imamu wa Ijumaa wa Michigan alisisitiza kuwa hatari kuu kwa Jamhuri ya Kiislamu inatoka ndani, si nje, na akaongeza: “Nguvu ya wananchi wa Iran imo katika umoja wao na kushikamana kwao na uongozi wenye hekima wa Ayatullah Khamenei. Umoja huu ndio heshima na rasilimali halisi ya Jamhuri ya Kiislamu.”

Akinukuu tofauti ya mitazamo kati ya mtazamo wa Kiislamu na ule wa Kimagharibi, alisema: “Magharibi inataka fadhila ziwe katika huduma ya siasa; lakini Jamhuri ya Kiislamu, kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, huweka siasa katika kuihudumia ya fadhila. Tofauti hii ni ya kimsingi na ya kimuundo.”

Mwisho, al-Shar‘ aliitaka mitazamo yote ya kisiasa kuepuka kuleta mivutano na badala yake kuelekea mshikamano, akiongeza: “Leo dunia inazisoma kauli za Kiongozi wa Mapinduzi na inachunguza jambo hili kama tukio muhimu. Namuomba Mwenyezi Mungu amhifadhi Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Iran, pamoja na wanazuoni wakuu na maulamaa wa Umma wa Kiislamu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha